contact

husen

Sunday, August 19, 2012

RAISI WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA ATANGAZA SIKU ZA MAOMBOLEZO


Baadhi ya miili ya wachimba migodi waliouawa na polisi Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kipindi cha maombolezo
nchini humo kufuatia mauaji ya wachimba madini thelathini na
 wanne yaliyofanywa na polisi,
wakati walipokuwa wakiandamana kudai malipo bora zaidi ya kazi.
Bwana Zuma pia ametaka tume ya uchunguzi ya kisheria ichunguze
mauaji hayo katika mgodi wa madini meupe yaani PLATINUM
 eneo la Marikana.
Wakati huohuo wachimba madini wameamriwa kurejea kazini
 siku ya Jumatatu la sivyo watafukuzwa kazi.
Lakini wengi wamesema kumaliza mgomo wao sasa ni sawa na
 kuwadhalilisha wenzao waliouawa.
Wanasema watarejea kugoma katika eneo la mgodi huo na wataendelea
 kushinikiza malipo bora zaidi ya kazi.
Hata hivyo chama cha wafanyakazi wa migodi cha NUM ambacho
kina uhusiano wa karibu na chama tawala cha ANC - kinasema
 wanachama wake wamekubali kurejea kazini.
Mmoja wa wachimba madini hao Vuyisile Mchiza, amesema
atarejea kazini iwapo idadi kubwa ya wenzake watakubaliana
 kusitisha mgomo.
''Iwapo idadi kubwa watarejea kazini kesho, basi na mimi
 nitakwenda''. Anasema. ''Iwapo wengi hawatakwenda kazini
nami pia sitakwenda, kwasababu sitaweza kufanya kazi wakati
 wengine wakiwa bado wanaomboleza''.

No comments:

Post a Comment