contact

husen

Wednesday, September 5, 2012

SUPER SPORT KUONESHA LIGI KUU TANZANIA BARA

.
Mwanga wa neema unazidi kuimulika ligi kuu ya Tanzania bara,
 baada ya kusaini mkataba mpya mzuri na Vodacom kwa miaka
mitatu, ligi hiyo inaelekea kupata udhamini kutoka kituo
 cha Tv cha Afrika kusini cha Supersport ambacho kitakua
 kinarusha live hizo mechi.
Ili kuweza kupata udhamini huo kumeandaliwa kipindi cha
 majaribio ya kurusha baadhi ya mechi za ligi msimu huu
 kupitia Supersport – ambacho kimepewa jina la
“Supersport week in Tanzania”.
Supersport kupitia majaribio hayo wataonyesha mechi zifuatazo:
Azam vs JKT Ruvu tarehe 28 mwezi huu,
 Simba vs Tanzania Prisons tarehe 29/9, African Lyon vs Yanga tarehe 30/9,
na mechi watani wa jadi Simba vs Yanga ya tarehe 3/10
Baada ya majaribio hayo kuna asilimia kubwa ligi kuu ya
 msimu ujao wa 2013/14 ikaanza kuonyeshwa na kituo hicho
 maarufu barani Afrika.
 
Stori kwa hisani ya Shaffih Dauda

No comments:

Post a Comment