Hatimaye matajiri wa London Chelsea
aka The Blues wakata kiu
kwa kutwaa ndoo ya klabu bingwa barani Ulaya
mara
baada ya
kuichapa Bayern Munich kwa penalti
4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani
ya
dakika 120, kwenye Uwanja wa
Allianz Arena, Munich, Ujerumani.
Tembo wa Ivory Coast Didier Drogba ndiye aliyekuwa shujaa wa
mchezo huo
kwani alikuwa na ujasiri wa
kuipatia The Blues mabao
mawili muhimu. Goli la
kwanza ikiwa dakika ya
88 aliposawazisha
mara baada ya Thomas Muller kuipatia
Beyern
goli dakika ya 83 ya mchezo
Arjen Robben alikwenda kupiga penalti
dakika ya 94 na kipa
Petr Cech aliyesema mapema amekwishasoma hatua za wachezaji
wa Bayern wakati wa
upigani wa penalti,
alidhihirisha hilo kwa
kupangua mkwaju wa winga huyo wa
kimataifa wa Uholanzi.
Cech kesho anasherehekea miaka 30 ya kuzaliwa kwake
Baada ya hapo, timu hizo zilishambuliana kwa zamu na kwa
tahadhari mno na hadi dakika 15 za kwanza zinamalizika
ubao wa matokeo ulibaki
kusomeka 1-1.
Dakika ya 107, Daniel Van Buyten alipata nafasi nzuri akiwa
anatazamana na kipa Cech, lakini shuti lake la
chini lilikwenda
nje sentimita
chache upande wa
kuliwa wa kipa huyo wa Chelsea
.mara baada ya
dakika 120
kumalizika ndipo Ndipo
walipoingia katika changamoto
ya mikwaju ya penati
Chelsea wakafuta machungu
ya 2008
walipofungwa
na Manchester United kwenye fainali mijni
Moscow
Waliofunga penalty za
Chelsea
ni David Luiz, Frank
Lampard na Ashley Cole, wakati Juan
Mata yake
iliokolewa Neur.
Kwa upande wa Bayern, waliofunga ni Lahm
, Gomez na
kipa Neur.
|
No comments:
Post a Comment