Wizara ya
Maliasili na Utalii imefafanua kuwa kwa mujibu wa
Sera ya Malikale ya mwaka
2008 (Kifungu cha 4.5 na 46),
wananchi, taasisi mbalimbali, pamoja na wadau
wengine wa
uhifadhi wanaruhusiwa kumiliki, kulinda, kuhifadhi na
kuendeleza
urithi wa utamaduni nchini kwa manufaa ya
kizazi cha sasa na kizazi kijacho kwa
sababu za mafunzo,
historia na utalii. Sera pia inaruhusu uwekezaji katika
maeneo ya malikale ambao unalenga kuhifadhi na
kutumia rasilimali za malikale
kama vivutio vya utalii.
Ufafanuzi huu
umetolewa kufuatia habari iliyoandikwa
na gazeti moja la kila siku kuhusu
mwekezaji kumilikishwa
isivyo halali eneo lenye magofu ya kihistoria la kisiwa
cha
Chole kilichopo wilayani Mafia ambayo sasa yanatumika
kama sehemu ya hoteli
ya kitalii.
Wizara kupitia
Idara ya Mambo ya Kale inatambua kuwa
magofu ya kihistoria katika kisiwa cha
Chole ni
Kumbukumbu za Urithi wa Utamaduni yenye umuhimu
kitaifa na kimataifa
na Magofu haya yanalindwa na Sheria
ya Mambo ya Kale Na. 10 ya mwaka 1964 na
marekebisho yake Na 22 ya mwaka 1979. Idara inawajibika
kusimamia uhifadhi na
uendelelezaji wake kulingana
na kanuni na miongozo ya uhifadhi na
uendelelezaji.
Wizara
inasisitiza kuwa siyo maeneo yote ya urithi wa
utamaduni yanasimamiwa na Idara
ya Mambo ya
Kale moja kwa moja. Maeneo ya urithi wa utamaduni
yenye sifa za
kitaifa ni mengi lakini 12 tu ndiyo yanayomilikiwa
na Serikali Kuu na
kuendelezwa na Idara ya Mambo ya Kale.
Maeneo yaliyo mengi yanamilikiwa na watu
binafsi,
taasisi za umma na binafsi na vijiji au wilaya.
Kwa mfano, Magofu ya
Chole, Mafia hayapo chini ya
umiliki wa Idara ya Mambo ya Kale moja kwa
moja
bali yapo chini ya umiliki wa wilaya
na serikali ya kijiji cha Chole.
|
No comments:
Post a Comment