Tarehe 23/05/2012
tuliandika makala inayosema:
‘Ay na B’Hits na urafiki uliochuja kimya
kimya’.
Makala hiyo ilijaribu kuangalia uhusiano wa
Ambwene Yesaya na
Hermy B ambaye ni
producer na mwenyekiti mtendaji katika kampuni
ya
B’Hits Music Group.
Hermy
B ambaye ameisoma makala hiyo, ametuandikia
barua kukanusha baadhi ya
mambo tuliyoyaandika
na pia kutoa ufafanuzi wa namna mambo
yalivyokuwa
na yalivyo sasa:
Ningependa
kujibu shutuma zilizoandikwa na
blog yako kuhusu uhusiano wangu na
swahiba
wangu A.Y. Ningependa ifahamike kwamba
mimi na A.Y kwa kipindi
cha miaka 4 tumefanya
kazi za muziki kwa karibu pamoja na kazi
nyingine
za biashara. Ni kawaida na inaeleweka
kwamba mahali popote watu
wanapofanya
kazi pamoja kugongana katika mawazo au
lugha ni jambo la
kawaida, na ndio changamoto
zenyewe. Si jambo la ajabu kama mimi na
swahiba wangu A.Y. kupishana katika kazi.
Baada
ya kusoma makala inayonihusu kwenye blog
yako nimeona ni umuhimu wa
kujibu ni makala yako
haswa kuhusu swali linalohusu utu na tamaa ya
pesa.
Kwanza ningependa ieleweke kwamba
umeniweka katika picha ya mtu
mwenye
tamaa kubwa ya pesa na nisiejali utu picha
amabayo imeanza
kunisumbua katika shuhuli
zangu kwa muda mfupi tu kwani wananchi
wameanza kuniona hivyo.
Hivyo
nimeona ni lazima nijibu kwani nikiiacha
bila kujibu madhara yake
yatakuwa mabaya.
Kwanza napenda uelewe sijawahi kuwa msimamizi
wa kazi
za A.Y zaidi ya kuwa producer wa
nyimbo zake tu. Kipindi chote hicho
nimekua
natumia utaalamu wangu kwenye kutengeneza
tu muziki wake.
Maswala mengine yoooote
amekuwa akifanya mwenyewe tena
bila msaidizi.
Pia
ufahamu bila A.Y na MwanaFA kunipa nafasi
kutengeneza muziki wao
nisingekua hapa nilipo.
Nadhani inaeleweka mahali popote duniani kwamba
kipaji ili kifahamike kwa watu lazima kipitie
kwa mtu fulani au mkondo
fulani. Si ajabu
kama kipaji changu cha kuproduce muziki
kimeweza
kufahamika kwa kupitia kwa A.Y.
Mimi sio mungu labda ningekua sehemu
nyingine
na mafanikio makubwa zaidi au machache zaidi,
lakini nachojua
rafiki yangu amenipa ngazi ya
kufika huku nilipo sasa, sijawahi kuficha
hilo
na hata wao wenyewe wanajua na bado
nashukuru kwa hilo.
A.Y
hajawahi kuingia mkataba wa aina yoyote
na kampuni ya BHits Music Group
Limited wala
mimi binafsi uliombana kufanya kazi na mimi na
sio mtu
mwingine yoyote. Nimetengeneza
nyimbo zisizopungua 30 za A.Y, kwa ajili
ya
albamu yake katika kipindi cha mwaka
2008 mpaka 2011. Baadhi ya
nyimbo hizo
zimeshatoka na nyingine bado zipo zikisubiri
uhitaji wake.
Wote tulikua na lengo la kutengeneza
muziki kwa wingi na kuuza kwenye
soko zuri la
muziki ili tufaidike kwa pamoja.
Muda
wote muziki ulikua unatolewa na unafanya
vizuri kwa radio na T.V na
show zilikua zinafanyika
na zote nilikua nazijua iwe ndani ya nchi au
nje ya nchi hii hata malipo nilikua nafahamu
ni kiasi gani na sijawahi
kufichwa na A.Y kuhusu hilo.
Utata
umekuja kwenye malipo yaliyotajwa kwenye
blog yako ambayo yameniudhi
sana na baadhi ya
wasanii wanaopenda kurekodi kwangu wameanza
kuwasiliana na mimi kuuliza bei imepanda lini na
kama inawahusu pia.
Kutoelewana
kwetu kwetu kibiashara ilikuwa mwezi
February mwaka huu yakihusu malipo
ya album hiyo.
Baada ya hapo niliamua kufunga mdomo wangu na
nisingesema chochote kwani haya yalikua yananihusu
mimi na rafiki yangu
tu. Nimeamua kuongea
sasa kwani nahisi nimeshambuliwa kwa
mara ya pili
kuhusu makubaliano haya na mara
ya kwanza niliamua kukaa kimya.
Kwanza
nataka ufahamu Katika kipindi cha kutokea
2008 mpaka leo hii (miaka 4)
kwa matumizi ya
nyimbo hizo, ambazo amekwishafanyia show
nje na ndani ya
nchi na nyingine kumpatia
nominations na tuzo tofauti, nilichowahi
kulipwa
hakitaweza kuzidi shilingi milioni tatu kwa
malipo ya awamu
tofauti kwa miaka minne.
Kilichotokea ni kwamba,
mwaka huu mwanzoni
kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na
mipango ya
kuzindua albamu yake. Na alitaka
kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu
akiwa na
mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango
wake binafsi pasi na
mimi. Nilishindwa kuelewa
nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo
mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa
kawaida anaehangaika kutoka.
Niliamua
kukubali kwamba ameamua kufanya
hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi
nikajaribu
kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu
ulikua
kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei
sawa ya kurekodi na msanii mkubwa,
kwani
hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada
ya kazi yoyote iwe ya
matangazo ama show huwa
hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni
kumi,
ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja
niliomba nilipwe millioni 2.
Akakubali
kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo
nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia
mkataba
wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae
aliona kwamba bei hiyo
kwake ni kubwa sana
hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana
meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na
niliona biashara hii itavunja
urafiki wetu.
Nilifikiria
sana kwamba nyimbo hizi nimekaa
nazo toka 2008 bila kuingiza chochote
na
maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu
urafiki wetu wa muda
mrefu kwa mabishano haya.
Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y
anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote
anazohitaji kwa albamu yake
BURE (bila malipo).
Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo
bado
hazijamixiwa, ila ampatie producer
mwingine amfanyie hiyo kazi.
Mpaka
naona hii makala A.Y hajaja kuchukua
hizo nyimbo na ndio naelewa kua
hayupo na
BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili
hajawahi kunipatia.
Huu ndio ukweli halisi.
Swala
la mimi kuwa na wivu na kinyongo na
mafanikio ya A.Y ni uongo na
nashangaa umetoa
wapi maneno hayo. Kama kulipwa kidogo,
huku nikiona A.Y
anaingiza fedha nyingi
kwa muziki tunaotengeneza pamoja basi
ningekua
nimegombana nae toka mwaka
2009 labda.
Narudia
kwamba nilikua najua kila show yake
inapofanywa na sikuwahi kujisikia
vibaya.
Nataka utambue pia nilikua na akili timamu
wakati nafanya kazi
na A.Y na muda wowote
nilikua na uwezo wa kubadili mawazo na
kutaka
tuandike makubaliano kwa karatasi
ila sikufanya hivyo na wala sijutii
chochote
kwa utaratibu wetu wa hatari wa kufanya kazi
bila mkataba wa
maandishi na ndio maana nipo
radhi hata sasa kumpatia nyimbo hizo bure
kama nlivomwambia hapo mwanzo. Nina meseji
zote na email
za mazungumzo yetu ambazo
nilihifadhi nikijua ipo siku nitaonekana mimi
ndie mkorofi, hivyo nachokisema nina
hakika nacho asilimia 100.
Picha
nyingine mbaya ulioichora ni kujaribu
kuonyesha kuna kutopendana kati
ya
maproducer. Mimi Master Jay na Marco Chali
ni marafiki wazuri tu na
mpaka leo hii nikiwa
na shida na nikamhitaji Marco Chali au Master
Jay
nitampigia simu bila aibu kwani hakuna
ugomvi kati yetu. A.Y, Master Jay
na Marco
Chali pia ni marafiki wa siku nyingi na katika
kipindi cha
miaka minne akiwa Bhits kwa
hiari yake na sio mkataba, A.Y amekuwa
akienda MJ records anapojiskia na mara kadhaa
mimi nimeenda na A.Y na
mara kadhaa
nimeenda peke yangu tena kwa ajili ya
shughuli zangu
binafsi.
Pia
ufahamu katika kipindi hicho A.Y alikua
akitumia muda mwingi MJ Records
kuliko
Bhits na hiyo yote ilikua ni mipango yake
binafsi. A.Y hajawahi
kuzuiwa kufanya kazi
na mtu mwingine kwani ni msanii huru.
Ndugu
yangu mimi ni mtu mpole nisiye na
ugomvi na mtu hapa mjini. Nasikitika
sana
kwa jinsi kwenye makala yako ulivyojitahidi
kuonyesha kwamba mimi
na swahiba wangu
tumejenga uadui.
Wasalaam
Hermes Bariki Joachim (Hermy B)
Managing Director
Source leotainment
No comments:
Post a Comment