Jeshi la Nigeria linasema limewaua watu saba wanaoshukiwa
kuwa wafuasi wa
kundi la wapiganaji wa Kiisalmu wenye
msimamo mkali la Boko Haram katika
mapambano kaskazini mwa nchi hiyo.
Msemaji wa jeshi hilo amesema watu wengine zaidi kumi
na watatu wamekamatwa
baada ya kushambulia kituo cha
ukaguzi cha jeshi, katika mji wa Maiduguri.
Ghasia hizo zimetokea siku moja baada ya polisi wa Nigeria,
kusema kuwa
wataanza kulinda kutwa-kucha, milingoti
ya simu za mkononi kufuatia milingoti
kadhaa kama hiyo
kushambuliwa mwezi uliopita, kaskazini mwa nchi.
Boko Haram ilisema ilifanya mashambulio hayo, kwa
sababu milingoti hiyo
inatumiwa kufuatilia
mawasilino baina ya wafuasi wake.
Akitoa maelezo ya tukio hilo la Maiduguri, Luteni Kanali
Sagir Musa amesema,
''Kundi la watu wenye silaha
wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Boko Haram
walishambulia
kituo cha ukaguzi cha kijeshi sehemu ambayo wanajeshi
walikuwa
wameweka kizuizi na kufanya ukaguzi.
Ramani ya Nigeria ikionyesha eneo la Maiduguri
''Wanajeshi walijibu shambulio hilo kwa risasi. Watu saba wenye
silaha
waliuawa katika majibizano hayo ya ufyatulianaji risasi,
na wengine kumi na
watatu walikamatwa huku
wengine wakikimbia. Hakuna majeruhi waliopatikana
kwa
upande wa wanajeshi.''
Boko Haram wanataka kuwekwa kwa utawala wa sheria
ya Kiislamu nchini
Nigeria.
Kundi hilo lilianzisha kampeni ya kijeshi mwaka 2009
kupigania kuanzishwa kwa
utawala wa Kiislamu, likishambulia
majengo ya serikali na makanisa na pia kuwaua
wahubiri wa
Kiislamu wenye msimamo wa kati.
Nchi hiyo imegawanyika kati ya eno la kaskazini lenye Waislamu
wengi na lile
la kusini linalokaliwa na Wakristo wengi na dini nyingine.
picha na stori kwa hisani ya bbc
No comments:
Post a Comment