contact

husen

Thursday, June 27, 2013

WATANZANIA WAISHIO MIKOANI WAPIGWA MARUFUKU KWENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA


Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.
Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa

Friday, June 21, 2013

MZIKI WAKE MNENE FIGA NAMBA 8

HATARIIII.....ANGALIA PICHA ZA MAJERUHI MAPOKEZI YA BECKHAM CHINA

Beckham stampedeVurugu tupu: Ofisa wa usalama na watu wengine wakijaribu kumbeba askari wa kike aliyepata majeruhi katika mapokezi hayo yaliyojaza nyomi kubwa san
David BeckhamKabla ya fujo: Maelfu ya watu wamejitokeza kumpokea nyoa Beckham katika chuo kikuu cha Shanghai
PolicewomanMaskini askari: Askari wa kiume akiwa amelala chini ya sakafu baada ya kujeruhiwa katika mapokezi hayo
Beckham crushFujo zaanza:  Maofisa wa polisi wameshindwa kuwazuia maelfu ya watu katika mapokezi hayoNa Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Nyota wa zamani wa Manchester United,  Los Angel Galaxy, Real Madrid, PSG na timu ya taifa ya England, David Beckham amewasili leo nchini China na kusababisha wanafunzi watano kujeruhiwa vibaya katika harakati za kumpokea  katika chuo cha Tongji University ambapo umati mkubwa ulifurika kupita kawaida.
Beckham ameenda kuwatembelea wanachama wa klabu ya mpira wa miguu ya chuo hicho kama sehemu ya ziara yake ya siku saba nchini humo yenye lengo la kuiamusha ligi kuu ya China.
Licha ya watu wengi waliofurika kuhitaji kushikana mikono na nyota huyo, imekuwa ngumu sana kulingana na watu kusukumana na kusababisha watu kujeruhiwa wakiwemo maaskari polisi.
Lengo la Beckham kuzungumza na wanachama hao limeshindwa kutimia kufuaia fujo hizo za watu wengi waliofurika, lakini ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook akiwaomba radhi mashabiki wake kwa kile kilichotokea.
Samahani sana jamani, nimeshindwa kuiona timu ya chuo kikuu pale uwanjani, kiukweli ilikuwa ngumu sana kupenya umati ule. Nimesikia watu wachache wamejeruhiwa, natumaini wanaendelea vizuri na nawatakiwa kheri wapone salama”. Alisema Beckham baada ya kuondoka uwanjani hapo.
Takribani watu elfu moja walikuwepo katika mapokezi hayo na kuhitaji kumshika nyota huyo,na tayari jeshi la polisi limethibitisha kuwa maofisa wake watu wamejeruhiwa katika fujo zoezi hilo.
Beckham mwenye umri wa miaka 38 amestaafu kucheza soka msimu uliopita ambapo aliwasaidia PSG kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa, Ligue 1.

MWIGULU NAYE ADAI KUWA BOMU LILIRUSHWA NA CHADEMA...."KAMA SIO WAO, MCHUKUA VIDEO ALITAARIFIWA NA NANI KWAMBA BOMU LITARUSHWA???"


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba  amesema bungeni leo kwamba Chadema ilipanga kufanya shambulio la bomu kwenye mkutano wa Soweto jijini Arusha.

Amesema hakuna jambo ambalo Chadema wamewahi kupanga wakashindwa.



“Itakuaje mtu amechukua mkanda wa tukio la umwagaji wa damu bila kutikisika au mchukuaji kukimbia, haiwezekani- hiyo walipanga.

“Inakuaje amechukua mkanda wa video kama mkanda wa harusi, yaani kama mkanda wa sendoff.? Amehoji Mwigulu huku wabunge wa CCM wakimuunga mkono kwa kupiga meza bungeni.


Mapema wiki hii katika mkutano wa Chadema, mtu mmoja asiyefahamika alirusha bomu kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha watu wanne  kufariki dunia na wengine 68 kujeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mt Meru, Arusha.

MWANAFUNZI APIGWA RISASI TUMBONI CHUO KIKUU CHA UDSM USIKU WA KUAMKIA LEO


Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao.
Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.
Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.
Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili chuoni hapo. Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini kinaendelea.
Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).
Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.

Wednesday, June 19, 2013

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKA WA ARUSHA


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetuma salamu za rambi mbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Muhongo kutokana na vifo vya wananchi watatu wa Mkoa huo vilivyotokea kufuatia mripuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto Jijini Arusha.

Watu wasiopungua 70 waliripotiwa kujeruhiwa wakati wa mripuko huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Soweto wa Chama cha Demokrasia ya Maendeleo { Chadema }.

Katika Taarifa ya rambi rambi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyotumwa kwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha na kutiwa saini na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alielezea kupokea kwa masikitiko na huzuni taarifa ya shambulio la kigaidi la bomu lililotokea tarehe 15 Juni mwaka 2013.

Balozi Seif alisema Taifa kwa mara nyengine tena limekumbwa na msiba wa njama za kigaidi zilizoua na kujeruhi rMkuu wa Koa wa Arusha aia wema wasio na hatia sambamba na tukio jengine linalofanana na hilo lililogharimu roho za wananchi wengine wakati wakiwa katika ibada Kanisani.

Balozi Seif alisema kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wananchi na yeye binafsi anatuma salamu hizo za rambi rambi kutokana na maafa hayo na kuwaombea marehemu malazi pema na majeruhi wapone haraka ili waungane na wenzao katika ujenzi wa Taifa.


Halkadhalika Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaiunga mkono Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kupambana na ugaidi wa aina yoyote hapa Nchini.

Alieleza kwamba SMZ na Wananchi wa Zanzibar wako pamoja na wenzao katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na maombolezo na kuwaomba wafiwa wawe na moyo wa ustahamilivu, uvumilivu na subra katika kipindi hichi.

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kutenga shilingi Milioni Mia Moja { 100,000,000/-} kama zawadi kwa kwa mtu ye yote atakayetoa Taarifa zitakazofanikisha kunaswa kwa mhalifu au watu wenye mtandao wa ulipuaji wa mabomu hapa Nchini.

JOHN MNYINKA ADAI KUWA KESHO WATAWASHA MOTO TENA JIJINI ARUSHA


WAKATI Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ikiendelea kumsaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema,Mbunge wa Ubungo John Mnyika kesho atawasha moto mwingine wa maombolezo uliotawanywa kwa mabomu jana.

Mnyika atakuwa msatari wa mbele kuongoza wafuasi wa Chadema kuaga miili ya watu watatu waliouawa katika shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Soweto.


Mbali na Mnyika zoezi hilo pia litasimamiwa na wabunge wanne wa Chadema walioachiwa huru kwa dhamana leo kwakua upelelezi wa kesi zao hazijakamilika.


wabunge hao waliachiwa huru kwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani hapo kabla ya kufikishwa Mahakamani na kutakiwa kurudi Polisi Julai 22 mwaka huu .


Wabunge hao Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu), walipewa dhama hiyo majira ya saa nane mchana.


Kabla ya Wabunge hao kuachiwa huru kwa dhamana, maelfu ya wafuasi wa Chama hicho walijazana katika Mahakama hiyo wakisubiri msafara wa wabunge hao, na mara baada ya kupewa taarifa kwamba wabunge hao wameachiwa huru wakiwa Polisi,maandamano makubwa yakaelekea katika Kituo cha Polisi.


Akizungumza baada ya dhamana hiyo Tundu Lissu alisema kwamba, Jeshi la Polisi limempa hasara kubwa baada ya kuvunja mawani yake na kwamba hivi sasa hawezi kufanya kazi yoyote mpaka atakapo pata mawani mapya.



Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliyefika jijini Arusha kwa ajili ya kuwawekea dhama wabunge hao alisema kwamba, Chama hicho bado kitaendelea na mipango yake ya kuomboleza na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu waliouawa kwa shambulio la bomu katika mkutano wa kisiasa wa Chama hicho Juni 15 mwaka huu katika Uwanja wa Soweto, marehemu hao ni pamoja na Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally, waliofariki kwenye mlipuko wa bomu.


Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutoka Polisi Mnyika alisema, "Kesho tutaendelea na zoezi la kuwaaga wenzetu waliofariki dunia katika mkutano wetu, na watazikwa kwa heshima zote za Chama,zoezi litaanzia kanisani kabla ya kwenda katika eneo maalum ilipoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho".


Hata hivyo Mnyika alikataa kujata jina la kanisa muda wala eneo iliyopangwa kwa madai kwamba ni mapema sana.

IDD SIMBA NA WENZAKE WAACHIWA HURU KATIKA KESI YA KUHUJUMU UCHUMI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo hii imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba pamoja na Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa Kata Sinza (CCM), Salum Mwaking’inda vile vile Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo.

Mahakama imewaachia huru washitakiwa kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi alliwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 28 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi.

Hivyo kuanzia sasa, washitakiwa hao wapo huru.

Monday, June 17, 2013

MAKAHABA WANAOJIUZA SINZA WATIWA MBARONI NA MGAMBO WA JIJI MCHANA KWEUPEE!!!








Mgambo wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika zoezi la kuwakamata akinadada wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu kama Machangudoa katika eneo la Sinza.

Picha hizi ( juu) zinaonesha namna walivyokuwa wakipakiwa ndani ya Gari tayari kwa kupelekwa katika vyombo vya sheria 

CHADEMA NA CCM WAKATANA MAPANGA MKOANI IRINGA CHADEMA NA CCM WAKATANA MAPANGA MKOANI IRINGA


MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wilayani Kilolo, Lunyiliko Nyaulingo amelazwa katika Hospitali ya mkoa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mgololo amelazwa Hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wanaodaiwa ni wanachama wa CCM katika kampeni za mwisho za kuwania nafasi ya udiwani.

Sambamba na hiyo Katibu wa CCM kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo, Wilhad Ngogo (40) na Yohana Mchafu anayedaiwa kuwa ni mwanachama wa CCM wanashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na matukio hayo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema watu hao walikamatwa jana kufuatia 
vurugu zilizojitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya mwisho katika wilaya hizo mbili.

Alisema kufuatia mzozo huo wanachama wa CHADEMA walizuia barabara ya Iringa-Mbeya kwa kuweka magogo ili kuzuia magari kupita na kuwa Polisi wanamtafuta Rabart Sam maarufu kwa jina la Kideri kwa kuongoza vurugu hizo.

Kamanda Mungi alisema wanafanya uchunguzi wa kina juu ya matukio hayo na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wote wa vyama vya siasa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kutokea.

Leo Uchaguzi wa udiwani katika kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo na Mbalamaziwa wilayani Mufindi ulifanyika ambapo Zuberi Nyomolelo (CCM) na Ezekiel Mlyuka (CHADEME) walipambana kwa kata ya Mbalamaziwa na kwa upande wa Ng’ang’ange Kilolo Nafred Chahe (CHADEMA) na Namgalesi Msuva (CCM) walipambana.

--
via Mjengwa

MWANAMKE AVUA NGUO NA KUCHEZA UCHI BAADA YA KUZIDISHA POMBE HUKO MBAGALA ZAKHEIM

 


DADA mmoja ambaye jina lake halikuweza kujulukana mara moja aliuacha hoi umati wa watu waliokuwa kwenye baa moja hivi (jina kapuni) huko mbagala Zakheim mara baada ya kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama na hivyo kusababusha hali ya taharuki katika maeneo hayo.
 
 

Chanzo cha habari  kinadai kuwa dada huyo alifika maeneo hayo akiwa vizuri kabisa...
Uchafu wake  ulianza baada ya yeye kunywa bia nyingi  mithiri ya mtu mwenye kiu ya maji .Pombe  ilipopanda kichwani, mrembo huyo alianza kukata mauno ovyo na  kusaula nguo mojamoja  mpaka  alipoyaanika na makalio yake..

 

PICHA: MWANAMKE ABAKWA NA KUZIKWA AKIWA HAI...POLISI WAMFUKUA NA KUKUTA AMEFARIKI





Matukio ya kikatili yameendelea kutikisa nchini Nigeria baada ya mwanamke mmoja kubakwa na kuzikwa akiwa mzima....

Taarifa toka katika mitandao ya kinigeria zinadai kuwa mwanamke huyo alibakwa na kisha wabakaji wakamfunga miguu na mikono.....

Zoezi la kumfukua likiendelea.....

Mwili wa dada huyo ukifukuliwa

Mwili umekwisha fukuliwa, bahati mbaya dada huyo amekwisha fariki....

Baada ya kumfunga,Mashetani hao walichimba shimbo porini walikotekeleza unyama huo na kisha kumzika akiwa hai ili kuficha ushahidi.....

Jeshi la polisi nchini humo lilifanikiwa kuipata habari hiyo masaa 12 baada ya mwanamke huyo kuzikwa akiwa hai....

Zoezi la kumfukua dada huyo lilianza, lakini bahati mbaya dada huyo alikuwa amekwisha fariki

KAMA ZAMANI "THE FINEST" NA MWANAFA @ MAKUMBUSHO YA TAIFA DAR ES SALAAM IJUMAA 14/6/2013


MwanaFA akitoa burudani kwa wahudhuriaji wa show ya "The Finest" Kama Zamani @ Makumbusho ya Taifa Dar Es Salaam Ijumaa 14//6/2013.

SINTAH AMTOLEA UVIVU OMMY DIMPOZ NA KUMPA LAKE LA ROHONI

Sinta ameandika haya yafuatayo katika website yake:

MDOMO UMEMPONZA HUYU KIJANA

"Daaah masikini akipata matako hulia mbwata, yaani nimesikitishwa na habari ya Ommy Dimpoz na kauli yake aliyotoa kwenye umma, hivi wewe Dimpozi unajua nini cha kuongea ktk public?? SMH usipende kuropoka ropoka tu hata kama wewe ukifa tutajuaje kwenye bank yako kuna kiasi gani acha kuongea kwasababu ya nyimbo tatu ,, Nainai, Badaye na Me n U, Angalia kijana na usiache mbachao kwa msala upitao sasa unajiliza nini katika radio na umeongea mwenyewe hivi hujui mdomo huumba na pia huponza kichwa??

sasa wewe unataka kuniambia u have invested na hutegemei show?? kumbuka sisi mashabiki wako ndio tumekuweka hapo juu na ku support music wako haya tukiacha kupenda nyimbo zako na ukakosa show itakuwaje??? umenizije sasa kumkejeli mwenzio tena kwenye kipaza sauti next time uliza nini cha kuongea ndio maana wenzenu wanakuwa na managers wa kuwa guide sio unaongea tu coz usikike. wenzio walionyamaza uliwaona mafala sio?? au ulitaka utoke kama hivi tukuongeleee cheap cheap fame.

kauli yako uko sahihi ila kwanini usingeiongelea ktk interviews zako kama ushauri kwa wasanii wenzio na ukaifanya ni big issue ktk msiba wa mwenzio??

nimekupa langu la roho kazi kwako sasa ukinichukia sijali, ukinipenda sawa coz naongea ukweli na wananchi waliokerwa wamenituma na sikuwepo ila wamerekodi wakaniambia CEO ifanyie kazi Ommy D katukwaza" says Sintah

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YA MAZISHI YA MSANII LANGA KILEO



DR. NCHIMBI AWAFARIJI WAHANGA WA BOMU NA KUTEMBELEA SEHEMU ILIYOLIPULIWA BOMU



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa katika viwanja vya Soweto Arusha palipotokea mlipuko wa bomu wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa katika viwanja vya Soweto Arusha palipotokea mlipuko wa bomu wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa katika viwanja vya Soweto Arusha palipotokea mlipuko wa bomu wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa katika viwanja vya Soweto Arusha palipotokea mlipuko wa bomu wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Askali wa JWTZ wakikagua gari la matangazo la chama cha chadema ambalo lilipigwa risasi kwenye tenki la mafuta lengo likiwa lilipuke, katika viwanja vya Soweto Arusha palipotokea mlipuko wa bomu na mashambulio ya risasi wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Askali wa JWTZ wakikagua gari la matangazo la chama cha chadema ambalo lilipigwa risasi kwenye tenki la mafuta lengo likiwa lilipuke, katika viwanja vya Soweto Arusha palipotokea mlipuko wa bomu na mashambulio ya risasi wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea wahanga wa mlipuko na shambulio la risasi vilivyotokea katika viwanja vya Soweto Arusha wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea waanga wa mlipuko na shambulio la risasi vilivyotokea katika viwanja vya Soweto Arusha wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea wahanga wa mlipuko na shambulio la risasi vilivyotokea katika viwanja vya Soweto Arusha wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea wahanga wa mlipuko na shambulio la risasi vilivyotokea katika viwanja vya Soweto Arusha wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea wahanga wa mlipuko na shambulio la risasi vilivyotokea katika viwanja vya Soweto Arusha wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea wahanga wa mlipuko na shambulio la risasi vilivyotokea katika viwanja vya Soweto Arusha wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea wahanga wa mlipuko na shambulio la risasi vilivyotokea katika viwanja vya Soweto Arusha wakati wa kufunga kampeni za kuwania udiwani wa kata za jijini arusha za chama cha CHADEMA
??????????????????????