contact

husen

Saturday, June 23, 2012

JOH MAKINI ATETA


Joh Makini amerudi kwa kishindo na ngoma yake 
iitwayo Manuva na iliyotengenezwa na mtayarishaji
 mkongwe Ambrose aka Dunga.

Tumepiga story na Joh Makini aka Mwamba
 wa kaskazini kuhusu masuala mawili
 matatu kama ifuatavyo.

Kuhusu wapi aliporekodi Manuva, anapoishi na 
anachofanya producer Dunga

Manuva tumeifanyia pale kwa Dunga nyumbani  ana 
microphone yake, amegonga beat nyumbani ana
 monitors (speaker) kwahiyo tukafanya pale, 
halafu tukaenda kufanya final mixing na 
mastering kwenye studio za B’Hits kwa 
Hermy B. Dunga anaishi Mikocheni. Anafanya
 production na kazi zake binafsi.

Kuhusu wasanii wa Hip hop kutopiga show 
za hela kama wanazofanya wasanii wa kuimba
 kama Diamond

Mimi nafikiri hiyo ni kwa wadau tu ambao industry
 wanaiona hivyo lakini kwa upande mwingine
 nafikiri watu wa hip hop pia wengi wako smart
 sana kibiashara na watu wenye misimamo
 mara nyingi,  sasa hiyo kwenye industry inakuwa
 kama shida fulani hivi.

Kuhusu mipango ya Weusi

Weusi tuna hii albam yetu ya pamoja ya Weusi,
 baada ya hapo kila mtu anaenda solo sasa, lakini
 kampuni inabaki pale pale kufanya biashara za
 Weusi kama kuuza nguo za Weusi na cds.

Kuhusu kama biashara hizo zinawalipa

Yeah inatulipa, faida ipo kwasababu tunanunua bidhaa, tunaitengeneza,tunauza kwa kiasi fulani cha
 hela ambacho kina faida pale juu yake, na sio
 mbaya inatusaidia kidogo mafuta ya gari na 
vitu vidogo vidogo kuendesha maisha. Sisi 
t-shirt zetu tunaziuza kwenye maduka ya watu
 tu yaani kama Born 2 Shine, kwa CP jembe pale
 Mwenge kwahiyo tuna washkaji zetu wenye
 maduka, tukitoa mzigo tunawapelekea kwenye
 maduka yao kwasababu nao wanapenda
 kusupport hip hop, kwahiyo tunafanya nao 
biashara kwa style hiyo.


Kuhusu kitu asichokipenda kwenye muziki wa sasa

Upigwaji wa nyimbo kwenye radio stations, nyimbo 
zinakuwa hazidumu. Wimbo unatolewa, unapigwa 
wiki,unapigwa wiki inayofuata wiki nyingine
 zinakuwa hazipigwi tena. Yaani hakuna upigwaji
 ambao unaweza kuufanya wimbo uishi. Kuna
 ngoma kama za Hip hop usipozipiga mara nyingi
 watu hawawezi kuelewa sababu utakuta kuna
 metaphors,mle ndani kuna mashairi magumu,
 mtu anatakiwa ayasikike mara mbili, mara tatu
 ili aweze kuyatafakari na kuyaelewa. Nadhani
 tunahiji airtime nzuri kwaajili ya watu kuelewa 
hiki tunachokuwa tunakiongea kwenye mistari yetu
 tofauti na wasanii wengine wa kuimba sababu wao
 muziki wao unategemea tu melody sio katika uandishi.
 Kwahiyo watu wakishapenda melody basi wimbo
 unahit lakini wimbo wa hip hop kama watu
 hawajaelewa maishairi inakuwa kidogo kazi.


SOURCE LEOTAINMENT

Friday, June 22, 2012

DOGO JANJA ATUA BONGO

Dogo Janja mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mwl Nyerere
International Aiport. Picha kwa hisani ya millardayo
Dogo Janja ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi 
na kusisitiza kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma 
Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile zilikua hasira tu
 hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho 
 amekikubali kwa roho safi. 

Janja amesema bado hajasaini mkataba mpya na 
WATANASHATI
 lakini kuna watu wake wawili anaowasubiri kwa ajili ya
 kuja kuupitia pamoja huo mkataba, baada ya hapo ndio
 atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza. 

Amesema amebadili mawazo na sasa atasoma Dar es salaam
 katika shule nzuri ambayo aliahidiwa na Ostaz Juma 
meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa shule na 
kurudishwa nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni
 kusoma kwenye shule binafsi nzuri na pia swala
 lake la muziki kuzingatiwa. 

kwenye sentensi nyingine amesema “sasa hivi
 nitakua naigiza na filamu pia na kina Kitale manake
 tuko nao kwenye kundi moja la watanashati”
Kwa kumalizia Janja amesema kauli mbiu ya wakati 
huu imebadilika “kauli mbiu ya wakati nilivyokujaga
 nilisema nawakalisha matembo sasa hivi
 nawalaza chali matembo”

Dogo Janja atasikika kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM 
kuanzia saa moja leo usiku utapata nafasi ya kusikia
 alichosema na jinsi alivyopokelewa kwa shangwe.
SOURCE DJ CHOKA

SOURCE DJ CHOKA

IZZO BIZNES FT SHASPIN - MWAKA JANA


SNOOP DOG NA WIZ KHALIFA KUTOKA NA MOVIE


Rapa Wiz Khalifa and Snoop Dogg wameamua kutengeneza movie
 itakayojulikana kama Mac And Devin Go To High School. Snoop
 Dog ameweza kufunguka na kuelezea ni kitu gani kilichomfanya
 apige kazi na Wiz Khalifa.

"Mac And Devin Go To High School ni movie ambayo
nimeifanya na Wiz ambaye nilipata chance ya kufanya na
e kazi katika ngoma ‘Black And Yellow Remix’ na pia alinitaka
 kufanya ngoma yake  katika albabam yake, kwahiyo kutokana
 na kufanya kwetu video kadhaandipo nikaja na wazo la
 kumuambia tukae chini na kutengeneza ngoma ambayo
 itatukumbusha maisha ambayo tuliishi high school" said Snoop

NGOMA SITA ZA KIBONGO ZILIZOFANYIWA SAMPLING TOKA MBELE


1.Fid Q na Lord Eyez – Neno

Producer – Samtimber
Wimbo waliosample: Coke Life wa G-Unit




 2. Ray C Ft Quick Racka – Nipe Love
Producer – Marco Chali
Wimbo waliosample: Easy – Paula Deanda





 3. Fid Q – August 13
Producer – P-Funk
Wimbo waliosample: Frozen – Madonna



 4. MwanaFa ft. Ay na Dully Sykes – Ameen
Producer – Dully Sykes
Wimbo waliosample – Hey – Cecile





5. Quick Racka – Fire Anthem
Producer – Bano
Wimbo waliosample – I’m Boss – Meek Mill ft. Rick Ross




6. Mabeste ft Jux – Sirudi tena
Producer – Pancho Latino
Wimbo waliosample – Champion – Chipmunk ft. Chris Brown





Thursday, June 21, 2012

KANUMBA KUENZIWA MAONYESHO YA SABA SABA

Bado mpaka sasa kumbukumbu za watanzania hazijalala, movie star

 marehemu Steven Kanumba bado anakumbukwa kwa sababu bado kazi zake

 nyingi alizozifanya zinaendelea kuonekana katika maisha ya kila

 siku ya watanzania wengi.

Wakati huu ambapo maonyesho ya sabasaba yanakaribia kuanza 

Dar es salaam familia yake imeamua kuchukua banda maalum

 kwenye viwanja vya saba saba kwa ajili tu ya kuendelea

 kumuenzi Marehemu Kanumba.


Seth ambae ni Mdogo wake waliekua wakiishi pamoja

 Sinza Dar es salaam amesema ni banda la Kanumba litakalokua

 na Nguo zenye alama alizokua anazitumia Kanumba ikiwa ni 

pamoja na jina na ujumbe, kutakua na picha zilizo kwenye frame za 

Kanumba zinazomuonyesha toka akiwa utotoni, pia vikombe, kanga

, bazee na vitu vingine vingi vyenye alama na picha za Kanumba.

Seth amesema Mama mzazi wa Kanumba pamoja na watu aliokua

 akifanya nao kazi Kanumba watakuwepo kutoa maelezo

 mbalimbali kuhusu Kanumba na kazi zake.

source millard ayo

RICK RSS - TOUCH 'N YOU FT. USHER


50 CENT ATOA MAONI JUU YA BIF LA CHRISS BROWN NA DRAKE

G. Unit C.E.O 50 Cent analinganisha
 beef ya Drake na Chris Brown
 iko kiraha sana na pia inawapaisha, akiongelea
 mzozo huo wakati 
akipiga story na LA Leakers, 50 cent
 hakujua chochote kuhusu hilo
 aliona picha ndipo aliposhangaa sana kusikia 
washikaji wamerushiana
 chupa katika club ya usiku huko New York.
 “Hivi ni kweli 
ule ugomvi umesababishwa na msichana? (Rihanna),
 Hapana sidhani basi wanakitu chao katika 
music wanajuana
 wenyewe” Alisema Fif. Ni mbaya sana sikudhani 
kama wanaweza
 kuhusishwa katika aina hiyo ya ugomvi, 
Meek Mill, Chriss Brown
 alafu Drake, sikuwahi kufikiria kati yao
 kuna mpiganaji, lakini
 ukiangalia itakuwa ni kimuziki sana sana” Aliendelea
 kufunguka Fid a.k.a Fif. 
 
source djfetty


DIAMOND MOYO WANGU IN LONDON


GODZILA FT CHEGE - HARDWORK PAYZ


DOGO JANJA KUTUA KWA OSTADH JUMA NA MUSOMA?

Dogo janja anatarajia kutua ndani ya dar siku ya kesho.  .
 The reason behind ni kwenda kucheki mkataba ambao ataingia
 na Ostadhi Juma na Musoma ili awe chini yake. Dogo janja amekwisha
 tumiwa tiketi ya ndege kwaajili ya safari hiyo ya kesho.Swali ni
 kwamba Dogo janja ana miaka 16 na kwa sheria za nchi motu
 ambaye hajafikisha miaka 18 haruhusiwi kuingia mkataba wowte. . 
 Katika hilo Dago amesema endapo atakubaliana na mkataba huo
 Baba yake mzazi ndiye atakayesaini kwa niaba yake.