contact

husen

Wednesday, May 23, 2012

KINJE KUTUA SIMBA

Nahodha  wa Klabu ya FC Leopards ya Kenya, 
Salim Kinje, anajiandaa kujiunga na mabingwa wa
 Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba ambapo ada 
yake inatizamiwa kuwa milioni 90 za kibongo.
Kiungo anatarajia kutua  Simba akipiga chini
 ofa iliyokuwa itolewe na Azam FC.
SuperSport.com wamesema mchezaji huyo ambaye
 amezivutia klabu nyingi za Tanzania, ataondoka
 na kujiunga na Simba kwenye usajili wa msimu
 ujao wa majira ya joto.
Imefahamika kuwa sababu kubwa ya mchezaji huyo
 kujiunga na Simba ni kuweza kupata nafasi ya 
kukichezea kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Kocha wa Leopards, Jan Koops, amethibitisha
 kuondoka kwa mchezaji huyo na kusema hataendelea
 tena kuitumikia timu hiyo.

No comments:

Post a Comment