contact

husen

Wednesday, May 23, 2012

MAOMBI YA KAJALA YAPIGWA CHINI KISUTU

Maombi ya msanii wa filamu nchini Kajala Masanja
 na mumewe Faraja Chambo ya kutaka kesi yao
 ihamishiwe kwa hakimu mwingine ili 
iweze kuendelea kusikilizwa yametupiliwa 
mbali na mahakama ya Hakimu mkaza 
Kisutu Dar es Salaam.
Maombi yao yalitupiliwa mbali na Hakimu Frank
 Moshi ambaye amesema amepokea jalada la
 kesi hiyo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi. Amesema
 amewasiliana na Hakimu Mfawidhi wa 
Mahakama Ilvin Mgeta ,na  amesema kwa
 kawaida shauri halifanyiwi mabadiliko
 iwapo hakimu yupo likizo na kwamba huo
 utakuwa ni usumbufu.Baada ya uamuzi huo
 alipanga kesi hiyo iahirishwe hadi Juni 5,
 mwaka huu itakapotajwa mpaka hakimu 
atakapomaliza likizo yake.
Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo 
wanakabiliwa na mashtaka matatu kula njama, 
kuhamisha umiliki wa nyumba na
 kutakatisha fedha haramu.

No comments:

Post a Comment