contact

husen

Wednesday, June 20, 2012

WASANII WA FILAMU WAPEWA CHANGAMOTO YA KUTOKA NA IDEA MPYA KATIKA KAZI ZAO


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Tasasi ya Gaba Arts 
mapema wiki hii wameendesha semina fupi kwa 
Wasanii wa filamu ili kuwajengea weledi katika
 eneo la uandishi bora wa miswada ya sinema
 (script writing).
Semina hiyo iliyoendeshwa kupitia programu 
ya Jukwaa la Sanaa kwenye Ukumbi wa BASATA 
ilijikita katika maeneo ya namna ya kuendeleza wazo 
hadi sinema ya kusisimua, namna ya kufikia 
hisia za watazamaji,ujenzi mzuri wa matukio,
kutengeneza wahusika na mfumo wa hadithi, Mwanzo,
 kati na hitimisho.

Akitoa mada kwenye programu hiyo maalum, Mkurugenzi 
wa asasi ya Gaba Arts James Gayo alisema kuwa, 
muda umefika sasa kwa wasanii wa filamu kusaka 
maarifa ili kutengeneza sinema zenye visa vipya, 
zenye weledi na zisizosukumwa na matakwa
 au maelekezo ya wasambazaji.
“Wenzetu kutoka nje wanatamani sana kupata 
vitu kutoka Afrika vyenye kuzungumza uhalisia 
wa maisha ya kwetu, wanataka kuona vitu vipya 
hivyo, katika uandishi wa muswada wa sinema suala 
la uhalisia na visa vyenye utofauti ni la msingi sana”
 alisisitiza Gayo.
Alizidi kueleza kuwa watazamaji wa sinema (filamu) 
huwa wana kawaida ya kuchoka pale wanapolishwa 
visa vya aina moja muda wote na akaonya kuwa
 kama wasanii hawatajikita katika kubuni visa vipya 
na vyenye kugusa uhalisia wa maisha yao wadau
 watasusia kununua.
“Ikiwa tutaendelea kutengeneza filamu zisizo na weledi,
 zenye visa vilevile na zenye kusukumwa na wasambazaji
 au haja ya kuchuma fedha za haraka tu watu 
watatuchoka na baadaye soko litakufa” alionya Gayo.

Gayo ambaye amepitia mafunzo ya utengenezaji
 filamu katika mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani
 alitaja sifa za muswada (script) bora kuwa ni
 pamoja na kubeba wazo linalozalika kwenye jamii,
 visa vyenye uhalisia na vipya, utengenezaji mzuri wa
 wahusika na sifa zingine nyingi.
Kwa upande wake msanii wa mashairi Mrisho Mpoto
 ambaye alikuwa miongoni mwa waliohudhuria
 semina hiyo alisema kuwa, wasanii wa filamu 
wanahitaji kusaidiwa kwani kwa sasa soko la filamu 
limekuwa la kitumwa na lenye kuburuzwa na
 matakwa ya wasambazaji bila weledi.

Akihitimisha programu hiyo, Katibu Mtendaji wa
 BASATA Ghonche Materego alishauri wasanii wa
 filamu kujipanga kushirikiana na wasomi wenye weledi
 katika maeneo yao ili kuzalisha kazi zenye weledi la ubora.
E
“Tuna wataalam wengi katika Sanaa, wamebanana
 na mambo mengi lakini ni vema wasanii 
tukawatumia na kushirikiana nao katika kuboresha
 kazi zetu” alisisitiza Materego.

source dj choka

KICHUPA CHA AY CHAFUNIKA MBELE MBELE


Siku chache baada ya kuachia video yake mpya ya ‘Party Zone’ msanii 
wa kimataifa wa nchini Tanzania, Ambwene Yesaya aka AY, vituo
 vikubwa vya runinga duniania vimeanza kuipiga video hiyo
 kwa fujo huku ikiipigia promo pia kwenye mitandao ya kijamii.
“Coming up on Crispy Fresh: Chris Brown, Coldplay ft Rihanna
, Kanye West, AY ft Marcochali ‘Party Zone’,Neyo, Usher &
 2freshLes,” iliandikwa jana kwenye ukurasa rasmi wa Twitter 
wa kituo cha Channel O cha Afrika kusini.
Kipindi hicho cha ‘Crispy Fresh’ hupiga video mpya zilizoifikia 
TV hiyo na katika lisi ya nyimbo hizi za jana kama zilivyotajwa kwenye
 orodha hiyo ni AY tu ndiye msanii kutoka Afrika ambaye wimbo wake
 upo katika awamu ya kipindi hicho na video zingine ni za wasanii wa Marekani.
Baada ya kuitambulisha video hiyo ambayo AY kamshirikisha 
Marco Chali, kituo hicho jana kiliandika tena, “Catch @AY ft Marcochali
 ‘Party Zone’ again at 17:43pm & 20:04pm on
 Channel O today, Original African.”
Wakati Channel O ikiendelea na promo hiyo ya video ya AY, 
kituo maarufu duniani kwa burudani cha nchini Ufaransa,
TRACE nacho kiliipa shavu video hiyo,
 “Comin up this hour— the brand new 
@Ay ft Marcochali – Party Zone! Stay tuned…”
Awali kabla ya jana TRACE Urban in Africa, iliitambulisha 
video hiyo kwa kuandika, “Stay tuned — coming up our
 EXCLUSIVE video – Ay ft marcochali “Party Zone” video!
 Only on TRACE Urban!”
Kwa promo hiyo ambayo ndo kwanza imeanza ni sahihi 
mtangazaji wa Clouds Fm Reuben Ndege kumuuliza hivi 
AY, “money still has a crush on you au tayari umeibebesha
 money mimba ya mapacha pair 4??? Na yeye kujibu.
 “Hahaha nishapiga mimba so big movement r gwan.”

source bongo 5

Tuesday, June 19, 2012

JAY Z NA KANYE WAFUNIKA NDANI YA PARIS


Jay Z na Kanye Westwamevunja rekodi yao kwa watu weusi 
kupiga show kali na iliyobamba ndani ya Paris katika 
The Throne tour. Wakali hao wamevunja rekodi ya
 hapo awali ambayo waliiweka takribani mwezi
 mmoja uliopita. Mapema wiki ijayo wawili hao
 watapiga show Sheffield, England ndani ya the 
Sheffield Arena na kumaliza tour yao ndani ya
 Birmingham, England's
 LG Arena

DIAMOND KUSUKUMA PRADO YA M 60






BONLOVE,VENTURE,MACKEY ON MKASI TV


MR BLUE AWA BABA

At last mpenzi wa Byser aitwaye Wahida 
amejifungua mtoto
 wa kiumena
 Mr Blue amempa jina la baba yake mzazi na 
kumuita SAMEER..
KWAFUJODEEJAYZ 
wish u all tha best



Monday, June 18, 2012

AMERUDI VS FLEXING ON EM UTATAAAAA

Kufuatia kuendelea kuwepo kwa zoezi 
la sampling za ngoma
 kadhaa hapa bongo hatimaye imegundulika 
ya kwamba ngoma
 ya Belle 9 amerudi mkono uliopigwa
 na Triss ni kama kuna 
sehemu flani ya kiitikio pale ambapo Belle
 anasema “ameruudi” 
ni kopy n paste toka katika ngoma ya 
Meek Mill - Flexin On Em
.Ngoma hiyo inapatikana katika mix tape 
“dackness nightmare”
Belle 9 amesema hakuwahi kujua kwamba
 beat ya amerudi
 imefanana na beat ya Meek Mill na
 isitoshe amerudi aliifanya
 2010 na Meek Mill ametoka juzi tu.
 Belle amesema alikuta
 beat hiyo studio akaipenda na kuamua
 kufanya nayo ngoma.
Upande wa pili wa shilingi Triss amesema 
alimsikia Belle akiimba
 “ameruudi” ndipo akapata idea ya
 kunyonga beat hiyo.
Hata hivyo Belle amekon clued kwa 
kusema ya kwamba idea
 huwa zinafanana coz muziki 
hauna mwenyewe

DRAKE APIGA SHOW JUMAMOSI

Drake amepiga show yake huko New York Beach Theater usiku wa
 jumamosi bila kupata bugudha yoyote kutoka kwa polisi ambapo
 kulikuwa na uvumi wa kwamba angekamatwa kufuatia
 kutokea kwa ugomvi kati yake na Chriss Brown na pia
 drake hakuzungumzia chochote juu ya ugomvi wake na
 Chriss Brown pamoja na mlinzi wake Big pat na
 Tony Parker anasumbuliwa na majeruhi mara baada
 ya kupigwa na chupa

CHRISS BROWN - DON'T WAKE ME UP



DJ WA CHRISS BROWN AMDIS DRAKE KATIKA TWEET YAKE



Saturday, June 16, 2012

DOGO JANJA APIGA MKONO NA JAMBO SQUAD

Dogo janja amepiga kolabo na krew ya Jambo Squad yenye
 makazi Ngarenaro. Pini hilo jipya linajulikana kama KIBOKO
 na ni mkono mpya kabisa toka Grand MastreZ

MHHHHHHHHHHHH


'ONE & ONLY' Video - Navio


AKAUNT FAKE YA JOKATE FACE BOOK YABAMBA


Mwanamitindo na mtangazaji wa kituo cha TV cha
 Channel O Jokate Mwegelo amesema amegundua 
kuwa akaunti fake ya Facebook ambayo inaonesha
 kuwa ni yake, ndio inayojulikana zaidi na yenye 
comments nyingi
 kuliko ile ya kweli.

‘So this fake fb a/c of mine has many more people making
 comments than the authentic one?!?...You fake and Ballin'
 smh...... #icant,’ aliandika jana.
“And the person gets like a hundred plus comments im like
 wooooow.....They need to be shut down.”

Jokate amesema yeye ana akaunti moja tu ya Facebook
 na zingine zenye jina lake si za kwake.

Baadhi ya watu wameshangaa kuona kuwa kuna watu
 wana muda wa kujifanya watu wengine kwenye mitandao
 ya kijamii utadhani hawana kazi za kufanya, “
so second account on fb is not urs. Wow!!People
 have time,” alitweet @MimiMimzamina.

Mbaya zaidi ni kuwa mtu huyo anayejifanya Jokate 
ameblock Jokate wa ukweli hivyo hawezi
 kufanya chochote.
“I swear yaani i was really shocked halafu huyo mtu 
mimi kani-block .”“I had managed to control
 one like two years ago will see what i can do
 with this one. Halafu the fake a/c katia i have a
 fb page like it kidoti classic, wowzerssssssss!!!!!
 so anayo mpaka page smh.....”

 
Akaunti yake halisi ya Facebook ina picha ya profile
 inayomuonesha akimbusu mama yake, picha ambayo
 anaitumia pia Twitter kama profile picture.
Watch out! There are lots of imposters
 out there!



SOURCE LEOTAINMENT

Wednesday, June 13, 2012

DOGO JANJA APIGWA CHINI TIP TOP


Nyota wa muziki wa kizazi kipya  kutoka  ‘kruu’ ya  Tip Top 
Connection  yenye maskani yake pande za  Manzese  jijini 
 Dar  es  Salaam  Abdul Abubakar Chende  ‘Dogo  Janja’
  ametupiwa  virago   ndani ya kundi hilo.
Akizumngumza mapema leo kiongozi wa kundi hilo
 Hamad Ally  ‘Madii’  amesema kuwa  Dogo Janja 
 ameshindwa  kuendana na  makubaliano halisi
 yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo
  kuhudhuria  shuleni kama alivyokuwa akitakiwa  kufanya
 kila siku  badala yake  amekuwa akiendekeza  starehe na
  wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja
 ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa  maeneo
 ya Ubungo tayari kwa safari ya  kurudi kwao  na wakati
 huo tulifanya mawasiliano na baba yake  kumuarifu kuwa
 Tip Top   hatuko na mwanae kwa sasa”  alisema Madii
Katika hatua nyingine Madii  amesema kuwa Dogo Janja
 alilewa sifa na  kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya
 ndani nanje ya kundi  kufuatia mafanikio ya muziki aliyoyapata
 akiwa  na Tip Top Connection kwani hivi karibuni alitega
 shule na kwenda kujificha  nyumbani kwa TundaMan
  hukua akimuaga Madii kuwa anakwenda shule.
Kuona hivyo TundaMan aliamaua kumuarifu Madii na
 mara moja  kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda
  kumsaka,  lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa
 Madii anakuja aliamua kukimbia na kwenda kujificha 
 uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni bahati mabaya  
alikanyaga  kuku  na  siri yake kujulikana kuwa amejificha
 hapao ndipo alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho
 chake  tayari kurejea ‘kileji’. vimekuwa ni vitendo vya 
kila mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na 
hatukuwa na njia nyingine ya kufanya alisema Madii'

SOURCE TEEN TZ

ONE - DEBUT [OFFICIAL VIDEO by DUKE GERVALIUS]


Tuesday, June 12, 2012

P-SQUARE FT RICK ROSS [Official Video]



TUNDAMAN NEW VIDEO


KICHUPA TOKA KWA BINAMU


DJ CHOKA AIBA TAULO HOTELINI

 Katika kipindi cha XXL kinachoruka kwa hewa week dayz toka 

7 kamili mchana hadi 10 za jioni katika gazeti la makorokocho

 the Gosip cop amenyaka tukio la uhalifu ambapo inasemekana 

ya kwamba Dj Choka aka Mr Hapetite kama anavyopenda kujiita

 ameiba taulo katika hoteli ya KUNDUCHI BEACH wakati msanii

 Linex alipokuwa

 akifanya video ya ngoma yake iitwayo AIFORA.


 Gosip Cop alimcheki Dj Choka kwenye simu yake ya mkononi 

 ndipo Linex alipotafutwa na kusema kwamba tukio hilo

 ni la kweli. .  lakini akamsihi Gosip Cop asitoe inshu hiyo

 hewani kwani dj Choka atamaindi.


 SOURCE XXL CLOUDS FM