contact

husen

Monday, June 11, 2012

HERMY B AFUNGUKA JUU YA KILICHOTOKEA KATI YAKE NA AY

Tarehe 23/05/2012 tuliandika makala inayosema:
 ‘Ay na B’Hits na urafiki uliochuja kimya kimya’. 
Makala hiyo ilijaribu kuangalia uhusiano wa
 Ambwene Yesaya na Hermy B ambaye ni
 producer na mwenyekiti mtendaji katika kampuni
ya B’Hits Music Group.

Hermy B ambaye ameisoma makala hiyo, ametuandikia 
barua kukanusha baadhi ya mambo tuliyoyaandika
 na pia kutoa ufafanuzi wa namna mambo
 yalivyokuwa na yalivyo sasa:

Ningependa kujibu shutuma zilizoandikwa na
 blog yako kuhusu uhusiano wangu na swahiba
 wangu A.Y. Ningependa ifahamike kwamba
 mimi na A.Y  kwa kipindi cha miaka 4 tumefanya
 kazi za muziki kwa karibu pamoja na kazi
 nyingine za biashara.  Ni kawaida na inaeleweka
 kwamba mahali popote watu wanapofanya
 kazi pamoja kugongana katika mawazo au
 lugha ni jambo la kawaida, na ndio changamoto
 zenyewe. Si jambo la ajabu kama mimi na
 swahiba wangu A.Y. kupishana katika kazi.




Baada ya kusoma makala inayonihusu kwenye blog
 yako nimeona ni umuhimu wa kujibu ni makala yako 
haswa kuhusu swali linalohusu utu na tamaa ya pesa.
 Kwanza ningependa ieleweke kwamba
 umeniweka katika picha ya mtu mwenye 
tamaa kubwa ya pesa na nisiejali utu picha
 amabayo imeanza kunisumbua katika shuhuli
 zangu kwa muda mfupi tu kwani wananchi
 wameanza kuniona hivyo.

Hivyo  nimeona ni lazima nijibu kwani nikiiacha
 bila kujibu madhara yake yatakuwa  mabaya. 
 Kwanza napenda uelewe sijawahi kuwa msimamizi
 wa kazi za A.Y zaidi ya kuwa producer wa
 nyimbo zake tu. Kipindi chote hicho nimekua
 natumia utaalamu wangu kwenye kutengeneza
 tu muziki wake. Maswala mengine yoooote
 amekuwa akifanya mwenyewe tena
 bila msaidizi.

Pia ufahamu bila A.Y na MwanaFA kunipa nafasi
 kutengeneza muziki wao nisingekua hapa nilipo.
 Nadhani inaeleweka mahali popote duniani kwamba
 kipaji ili kifahamike kwa watu lazima kipitie
 kwa mtu fulani au mkondo fulani. Si ajabu
 kama kipaji changu cha kuproduce muziki
 kimeweza kufahamika kwa kupitia kwa A.Y.
 Mimi sio mungu labda ningekua sehemu nyingine
 na mafanikio makubwa zaidi au machache zaidi,
lakini nachojua rafiki yangu amenipa ngazi ya
 kufika huku nilipo sasa, sijawahi kuficha hilo
 na hata wao wenyewe wanajua na bado
 nashukuru kwa hilo.

A.Y hajawahi kuingia mkataba wa aina yoyote
 na kampuni ya BHits Music Group Limited wala
 mimi binafsi uliombana kufanya kazi na mimi na
 sio mtu mwingine yoyote. Nimetengeneza
 nyimbo zisizopungua 30 za A.Y, kwa ajili ya
 albamu yake katika kipindi cha mwaka 
2008 mpaka 2011. Baadhi ya nyimbo hizo 
zimeshatoka na nyingine bado zipo zikisubiri
 uhitaji wake. Wote tulikua na lengo la kutengeneza
 muziki kwa wingi na kuuza kwenye soko zuri la
 muziki ili tufaidike kwa pamoja.

Muda wote muziki ulikua unatolewa na unafanya
 vizuri kwa radio na T.V na show zilikua zinafanyika
 na zote nilikua nazijua iwe ndani ya nchi au
 nje ya nchi hii  hata malipo nilikua nafahamu
 ni kiasi gani na sijawahi kufichwa na A.Y kuhusu hilo.

Utata umekuja kwenye malipo yaliyotajwa kwenye
 blog yako ambayo yameniudhi sana na baadhi ya
 wasanii wanaopenda kurekodi kwangu wameanza
 kuwasiliana na mimi kuuliza bei imepanda lini na
 kama inawahusu pia.

Kutoelewana kwetu kwetu kibiashara ilikuwa mwezi
 February mwaka huu yakihusu malipo ya album hiyo.
 Baada ya hapo niliamua kufunga mdomo wangu na
 nisingesema chochote kwani haya yalikua yananihusu
 mimi na rafiki yangu tu. Nimeamua kuongea
 sasa kwani nahisi nimeshambuliwa kwa 
mara ya pili kuhusu makubaliano haya na mara
 ya kwanza niliamua kukaa kimya.

Kwanza nataka ufahamu Katika kipindi cha kutokea
 2008 mpaka leo hii (miaka 4) kwa matumizi ya
 nyimbo hizo, ambazo amekwishafanyia show
 nje na ndani ya nchi na nyingine kumpatia
 nominations na tuzo tofauti, nilichowahi kulipwa
 hakitaweza kuzidi shilingi milioni tatu kwa
 malipo ya awamu tofauti kwa miaka minne.
 Kilichotokea ni kwamba, mwaka huu mwanzoni
 kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na
 mipango ya kuzindua albamu yake. Na alitaka
 kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu akiwa na
 mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango
 wake binafsi pasi na mimi. Nilishindwa kuelewa
 nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo
 mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa
 kawaida anaehangaika kutoka.

Niliamua kukubali kwamba ameamua kufanya
 hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi nikajaribu
 kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu
 ulikua kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei
 sawa ya kurekodi na msanii mkubwa, kwani 
hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada
 ya kazi yoyote iwe ya matangazo ama show huwa
 hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni kumi,
 ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja
 niliomba nilipwe millioni 2.

Akakubali kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo
 nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia mkataba
 wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae 
aliona kwamba bei hiyo kwake ni kubwa sana
 hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana
 meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na
 niliona biashara hii itavunja urafiki wetu.

Nilifikiria sana kwamba nyimbo hizi nimekaa
 nazo toka 2008 bila kuingiza chochote na
 maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu
 urafiki wetu wa muda mrefu kwa mabishano haya.
 Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y
 anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote
 anazohitaji kwa albamu yake BURE (bila malipo).
Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo 
bado hazijamixiwa, ila ampatie producer
 mwingine amfanyie hiyo kazi.

 Mpaka naona hii makala A.Y hajaja kuchukua
 hizo nyimbo na ndio naelewa kua hayupo na
 BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili
 hajawahi kunipatia. Huu ndio ukweli halisi.

Swala la mimi kuwa na wivu na kinyongo na
 mafanikio ya A.Y ni uongo na nashangaa umetoa
 wapi maneno hayo. Kama kulipwa kidogo,
 huku nikiona A.Y anaingiza fedha nyingi
 kwa muziki tunaotengeneza pamoja basi
 ningekua nimegombana nae toka mwaka
 2009 labda.

Narudia kwamba nilikua najua kila show yake
 inapofanywa na sikuwahi kujisikia vibaya.
 Nataka utambue pia nilikua na akili timamu
 wakati nafanya kazi na A.Y na muda wowote
 nilikua na uwezo wa kubadili mawazo na
 kutaka tuandike makubaliano kwa karatasi
 ila sikufanya hivyo na wala sijutii chochote
 kwa utaratibu wetu wa hatari wa kufanya kazi
 bila mkataba wa maandishi na ndio maana nipo
 radhi hata sasa kumpatia nyimbo hizo bure
 kama nlivomwambia hapo mwanzo. Nina meseji
 zote na email za mazungumzo yetu ambazo
 nilihifadhi nikijua ipo siku nitaonekana mimi
 ndie mkorofi, hivyo nachokisema nina
 hakika nacho asilimia 100.

Picha nyingine mbaya ulioichora ni kujaribu
 kuonyesha kuna kutopendana kati ya
 maproducer. Mimi Master Jay na Marco Chali
 ni marafiki wazuri tu na mpaka leo hii nikiwa
 na shida na nikamhitaji Marco Chali au Master
 Jay nitampigia simu bila aibu kwani hakuna
 ugomvi kati yetu. A.Y, Master Jay na Marco
 Chali pia ni marafiki wa siku nyingi na katika
 kipindi cha miaka minne akiwa Bhits kwa
 hiari yake na sio mkataba, A.Y amekuwa
 akienda MJ records anapojiskia na mara kadhaa
 mimi nimeenda na A.Y na mara kadhaa
 nimeenda peke yangu tena kwa ajili ya
 shughuli zangu binafsi.

Pia ufahamu katika kipindi hicho A.Y alikua 
akitumia muda mwingi MJ Records kuliko
 Bhits na hiyo yote ilikua ni mipango yake
 binafsi. A.Y hajawahi kuzuiwa kufanya kazi
 na mtu mwingine kwani ni msanii huru.

Ndugu yangu mimi ni mtu mpole nisiye na
 ugomvi na mtu hapa mjini. Nasikitika sana
 kwa jinsi kwenye makala yako ulivyojitahidi
 kuonyesha kwamba mimi na swahiba wangu
 tumejenga uadui. 

Wasalaam
Hermes Bariki Joachim (Hermy B)
Managing Director

Source leotainment

Sunday, June 10, 2012

MISS MONDULI 2012 MARRY MOLEL



Miss Monduli Marry Molel akipokea taji la maua toka kwa Regina Lowasa

Top 5 ya  warembo. .  kutoka kushoto Esther Thobico, Sauda Shabani,

 Mary Molel,

Sonia Kamara, Mesiana Samwel

 

Jumla ya washiriki 10 waliojitokeza katika kinyang'anyiro cha kumsaka

  mlimbwende wa Wilaya ya monduli hatimae jana usiku mshindi kapatikana na

  kuvishwa taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya Monduli. Tukio

 hilo la kihistoria lilishuhudiwa live na mamia ya wakazi pamoja na mgeni

 rasmi akiwa ni mke wa mbunge wa monduli Mama Regina Lowasa

Friday, June 8, 2012

KICHUPA KIPYA CHA WAKALI KWANZA FT KEKUU


MREMBO ATAKAEWAKILISHA JIMBO LA MONDULI KUFAHAMIKA LEO


Kinyang'anyiro cha kumtafuta mrembo mkali kuliko wote monduli 

 leo kitakua kikitimua vumbi katika ukumbi wa chuo cha

 ualimu monduli kuanzia majira ya saa kumi na mbili jioni, 

warembo kumi watapanda jukwaani kuonyashana kazi

 mbele ya majaji

Tuesday, June 5, 2012

SHAA AWACHUKULIA OYA OYA UWAZI

Gazeti hilo lililotoka leo (June 5) lina kichwa cha habari kisemacho
 "Master Jay & Shaa wamwagana. Babu Tale atajwa
 kuwa chanzo,
 Master Jay aelezea kilichotokea."

Akiwa amemkopi @masterjtz , Shaa ameandika
 “Woke up to this...cute! For show bookings,interviews
 and all plz contact Babu Tale.”


Gazeti la uwazi linasema wapenzi hao wameachana kisa Babu Tale.
 Hata hivyo Shaa ameendelea kusisitiza juu ya watu
 wanaotaka kufanya show naye wawasiliane na Tale
 ambaye inavyoonekana ni meneja wake.
Wakati Master Jay yuko busy na EpiqBSS, snitches
wako busy kuiangalia ‘Siri ya Penzi’ kati yake
na Shaa. 

SOURCE LEOTAINMENT


MAGRETH ZZIWA SPIKA MPYA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Monday, June 4, 2012

HOPE FOR TANZANIA WATOA MSAADA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 15


Shirika lisilo la kiserikali la Hope For Tanzania limetoa computer 92
 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 kama 
mchango wa kuinua kiwango cha elimu katika
 shule nne jijini Arusha.
 Wakurugenzi wa shirika hilo hapa Tanzania Felex Masenge
  na Naomi Masenge wamesema kuwa msaada huo
 unatokana na wafadhili wa shule isiyo ya kiserikali ya
 Tuishime ambao waliahidi kuzisaidia shule 10 jijini
 arusha vifaa hivyo  ili wanafunzi waweze
 kujifunza somo la Tehama.
Felex amesema kuwa zoezi hilo la kupatiwa computer 
 linaendelea hali ambayo itatoa fursa kwa shule
 hizo kufanya vizuri kielimu katika ulimwengu
 wa sasa wa sayansi na teknolojia.
Akikabidhi computer  hizo kwa wakuu wa shule
 hizo ambazo ni shule ya msingi uhuru,ukombozi
,kijenge na tuishime mgeni rasmi  katika  hafla hiyo 
Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema
 kuwa vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka na
 amewataka kuvilinda na kuvitunza vizuri.
Pia amesema kuwa shule nyingi za serikali zinakabiliwa
 na changamoto ya ukosefu wa fedha  hali ambayo
 inapelekea kushindwa  kununua computer  na wanafunzi
 kushindwa kufanya mitihani ya Tehama kama ilivyo
 kwa  shule  zinazomilikiwa na watu binafsi.
Aidha Augustino ametoa wito kwa wakuu hao wa
 shule kuzitunza na kuzilinda  na kuwa hatokuwa
 tayari kupokea taarifa ya  kupotea ama kuibiwa 
kwa vifaa hivyo   bali hatua kali za kisheria
 zitachuliwa dhidi ya mwalimu husika.
Lakini hata hivyo amewataka walimu kwenda
 shule na kwenda kujifunza alimu ya computer ili
 waweze kuwafundisha wanafunzi somo hilo la Tehama
 na hatimaye waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Akionge kwa niaba ya wakuu wa shule diwani wa kata ya
 sokon one Michael Kivuyo amesema kuwa ni vyema
 watanzania wakaiga mfano huo kwa kuchangia kuinua
 elimu katika shule za msingi na sio kuchangia ama kutoa
 msaada kwa mambo yasiyo ya msingi katika jamii

Sunday, June 3, 2012

MAISHA YA HOSNI MUBARAK KUISHIA JELA

Mahakama nnchini Misri imemuhukumu  aliyekuwa a rais wa nnchi
 hiyo Hosni Mubarak kifungo cha maisha jela kwa makosa mbali mbali
 ikiwemokuamrisha mauaji kwa waandamanaji waliokuwa wakiipinga
 serikali yake...Hata hivyo watoto wa mtwala huyo wa kijeshi wa
 zamani wameachiwa  huru pamoja na baadhi ya maafisa wengine
 wa Mubarak huku waziri wa zamani wa mambo ya ndani naye
 akikutwa na adhabu kama ya Mubarak.Akisoma hukumu hiyo
 jaji aliyetoa hukumu alisema mubarak akisababisha giza misri
 na kusababisha nchi hiyo kuwa moja kati ya nchi maskini duniani
 Alizaliwa mwaka 1928 katika kijiji kidogo  katika jimbo la
 Menofya karibu na jiji la Cairo...Pia Mubarak alikuwa akisisitiza 
usiri mkubwa wa historia yake na habari zake kwa ujumla.
Mubarak alimuoa mwanamke mwenye asili ya kiingereza 
Suzane Mubarak na kufanikiwa kupata watoto wawili 
ambao ni  Gamal na Alaa,
Mubarak alifahamika kwa utendaji wake wa nguvu na ukakamavu
 kwani ratiba yake ilikuwa ikianza saa kumi na mbili asubuhi kila
 siku, Hakuwa akinywa pombe wala kuvuta  sigara badala yake
 kwenye ujana wake alikuw akijihusisha na gym na
 kucheza mchezo wa squash.

Madaraka
Muhhamad Hosni Sayyid Mubarak aliapa rasmi 14/10/1981
 siku nane baada ya mauji ya aliyekuwa rais wa nnchi hiyo
 Anwar Saadat huku akiwa ni rais wa nne wa nnchi hiyo na katika 
kipindi chote alichokuwa madarakani aliliweka taifa hilo chini ya 
udharura (state of ermegence) na Hakusita kuwanyamazisha
 wapinzani wake kisiasa   na hata kuwafunga.Mubarak alikuwa
 alipoingia tu madarakani aliiingiza nnchi hiyo katika utawala wa
 kijeshi.Toka 1981 alipoingia madarakani  alishinda chaguzi tatu 
 zisizo na upinzani na baada ya kupewa shinikizo mwaka 2005
 alibadilisha mfumo na kuruhusu wapinzani huku yeye na chama 
chake cha NDP wakionekana dhahiri kupendelewa na
 kukandamiza upinzani hsa chama cha MUSLIM BROTHERHOOD 
Mubarak alikuwa mmoja kati ya viongozi waliotwala muda
 mrefu zaidi duniani na pia amekuwa kiongozi wa kwanza kutoka 
nnchi zilizokumbwa na vugvugu za kisiasa kuhukumiwa mahakamani.

 Wananchi wa Egypt wakiwa Tahrir Square
 baada ya hukumu ambayo
 imeacha vurugu kubwa Cairo na Alexandria.

  Source Thecommunity TZ

Friday, June 1, 2012

NICKI AKANUSHA UVUMI WA DANCER WAKE KUMUUA FANS WAKE HUKO JAPAN

Nicki Minaj akiwa stage kwenye tour yake ya Pink Friday huko Japan 
Picha ndogo ni msichana Nikola Furlong Ambaye ameuwawa na
 dancer wa Nicki aitwaye Larry

The Arajuku Beibe  Nicki Minaj kutoka YMCMB akanusha kuwa moja kati
 ya madencer wake ndio walihusika na kifo cha Nicola Furlong  siku ya tarahe 
 25 mwezi May kwenye chumba cha Hotel ya Tokyo hotel,  alipokuwa kwenye
 tour yake  ya Pink Friday Tour iliyofanyika Mjini Japan
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 aliyefahamika kwa jina
 la Nicola Furlong
 ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Dublin City University in
 Ireland alikutwa
 amekufa kwenye chumba cha hotel lisaa limoja mara baada ya show
 ya Nicki minaj kumalizika na mtu ambaye anasadikika kuondokanae
 mara ya mwisho ni dancer wa nicki minaji anayefahamika kwa jina la Larry
. “Sizani kuwa madencer wangu ndio wamefanya hicho kitendo kama watu
 wanavyo publish ila uchunguzi wa polisi utakapo kamilika ndio tutajua
 kuwa nini kilitokea mpaka kusababisha kifo cha Nicola ambaye alikuwa
 ni moja kati ya mafans wangu” Nick alimalizia kwa kutoa pole kwa familia
 ya marehemu Nicola, Mpaka sasa watu wawili ndio washikiliwa na
 polisi na inasemekana wote ni Madencer wa Nick minaj japokuwa
 Nick anakanusha kuwa mmoja kati ya watu hao wanaoshikiliwa
 sio Dancer wake na wala hamfahamu…..

JAMAA AFANYA MAUAJI YA KINYAMA SOUTH BEACH



Hatimaye ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, Polisi huko
 South Beach wamepata sura ya kijana aliyewauwa watu wawili mmoja
 alimchinja na mwengine alimtoboa macho akamkata pua pamoja na mdomo,
Kijana huyo ambaye sura yake imekuwa gumzo marekani nzima
 alitekeleza kitendo hicho cha kinyama siku chache zilizopita
 na kwa uchunguzi wa polisi inasemekakabla ya kuwauwa aliwaingilia 
kinyume na maumbile,

Jamaa aliyefanya unyama huo