contact

husen

Saturday, May 26, 2012

KELVIN McCAL FT BIG SEAN- NAKED


KUTOKA RISASI



SIMBA, MAZEMBE NA APR KUMUENZI MAFISANGO

Mabingwa wa  soka Tanzania bara Simba Sports Club 
aka Mnyama kwa kushirikiana na klabu za
 Tp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
 Congo DRC  pamoja na APR ya Rwanda, zipo katika
 mchakato wa kuandaa mechi maalum kwa ajili
 ya kumuenzi aliyekuwa mchezaji wao, 
Patrick Mutesa Mafisango.
Mafisango ambaye alifariki dunia wiki iliyopita jijini 
Dar es Salaam kwa ajali ya gari alizikwa nyumbani
 kwao Kinshasa, Congo.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 
 amesema jana kwamba, hawana budi kumuenzi
 mchezaji huyo kutokana na kutoa mchango mkubwa
 kwa timu hizo enzi za uhai wake.
Aliongeza kuwa fedha zitakazopatikana zitapelekwa
 katika familia ya Mafisango ili ziweze kusaidia wake 
na watoto wake.
Aidha, Simba imezishukuru timu za Yanga
 kupitia wazee
 wa baraza, Azam Fc, Coastal Union,
 Villa Squad ,
 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom na
 Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
 Kilimanjaro kwa michango yao ya hali na 
mali baada ya kutokea kwa msiba huo.

MISS UNIVERSE TANZANIA 2011 KUSAIDIA WANAWAKE WENYE KANSA YA MATITI



Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu anatarajua kufanya

 harambee ambayo itafanyika kataika Hoteli ya Serena jijini

 Dar es Salaam lengo kubwa ikiwa ni kuwasaidia wanawake

 wanaosumbuliwa na kansa ya matiti kwa kutumia 

 fedha itakayopatikana katika harambee hiyo

MKUTANO AFDB KUGHARIMU BILIONI 12


 Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB)inatarajia kutumia
 kiasi cha Shilingi bilioni 12 katika mkutano wake unaoanza 
Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi
 Jakaya Kikwete  huku kiasi cha fedha hizo zikitumika 
kukarabati Kumbi mbalimbali za jengo la Kimaitaifa
 la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya kumbi za
 jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana 
na utandawazi uliopo kwa sasa ndani ya nchi zilizoendelea
Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari
 mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mkutano wa benki
 ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha  Magonya  
ambapo alisema kuwa mkutano huo
 utakuwa na faida kubwa sana

Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo ambao utaanza
 Jumatatu ijayo utakuwa na faida kubwa sana kwa
 jiji la Arusha kwa kuwa hata kiwango cha uchumi
 kitaaimarika sana kwa kuwa wageni mbalimbali
 kutoka katika maeneo ya nchi mbalimbali
 duniani watabadilishana hata uzoefu

“kwa kipindi hiki ambacho kuna mikutano ndani ya jiji la
 Arusha tunatarajia kuwepo na utoafuti wa khali ya juu 
sana hasa katika mchakato wa uchumi na kwa hali hii pia
 tunatarajia hata kufanya maendeleo mbalimbali  ikiwemo
 kufanya marekebisho kwa jengo la kimataifa la AICC”
alisema bw Magonya

Katika hatua nyingine alifafanua kuwa mbali na kuweza 
kuimarisha uchumi wa mkoa wa Arusha pia wanatarajia
 kutumia fursa mbalimbali za kuhakikisha kuwa 
wanakutanisha wafanyabiashara mbalimbali huku
 malengo yakiwa ni kuendeleza uchumi
 kwa walengwa.

Pia alifafanua kuwa mbali na kuweza kuwasaidia
 wafanyabiashara hao katika michakato ya kukuza
 uchumi pia benki hiyo ina mikakati mbalimbali ya
 kuendeleza barabara ambazo zitaweza kutumika kama
 njia ya mawasiliano hapa Tanzania hali ambayo nayo
 itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuimarisha
 uchumi wa nchi ya Tanzania

Aliongeza kuwa hapo awali benki hiyo ilikuwa imeshajenga
 barabara ya Arusha –Namanga kwa sasa ana mpango wa
 kujenga barabara ya Arusha – Holile ndani ya Mkoa wa
 Kilimanjaro hali ambayo itachangia sana maendeleo
 hasa ya mawasiliano

Alimalizia kwa kusema kuwa wafanyabiashara hasa 
wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa 
wanatumia vema fursa za mkutano huo ili kuweza
 kuimarisha biashara zao za kila siku.

Friday, May 25, 2012

JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LAKAMATA MAGUNIA 50 YA BANGI

Watu  wanne waliofahamika kwa majina ya
 Babuu Laizer, Lomnyika Lekibengi, John Joshua, 
Edward Moleli wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani 
Arusha kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya
 aina ya bangi katika magunia 50.
 Kwa mujibu wa maelezo ya 
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Thobias Andengenye 
 amesema watu hao wamekamatwa wakiwa na gari aina ya
 Center DCM lenye namba za usajili T922 AFJ huko
 Vilima Saba Wilayani Longido katika Mkoa wa Arusha
 walipokuwa wakisafirisha bangi hiyo kuipeleka 
huko Nairobi Nchini Kenya, watu hao wanatarajia
 kufikishwa mahakamani siku ya jumanne

KICHUPA CHA AY ALICHOKIFANYA SAUZ CHAKAMILIKA


 Kazi ya kushoot video ya Ambwene Yesaya aka AY iliyofanyika jijini
Johannesburg, Afrika Kusini imemalizika salama jana.
AY aliambatana na producer wa wimbo huo uliokuwa ukifanyiwa video,
Marco Chali wa Mj Records.
Video hiyo ambayo kwa mujibu wa AY imegharimu $20,000 ambazo ni
zaidi ya shilingi milioni 30 za Tanzania, imeongozwa na director wa
Nigeria anayeishi nchini Afrika Kusini Mike
 Wakati wa shooting hiyo wanamuziki mapacha wa kundi la P-Square,
Peter na Paul Okoye walikuwepo japo haijulikani kama wataonekana
kwenye video ya AY kwakuwa nao walikuwa wakifanya video yao na
kampuni hiyo.
Baada ya kukamilisha shughuli hiyo AY alitweet,” I_Am_Godfather are
very professional,great team EVER,we gonna shoot more videos with
them.”
“Had a great shoot with Tanzanian hottest artist, @AyTanzania! #its a
wrap! Good working with you sir!” aliandika mmoja wa watu
waliohusika kushoot video hiyo.

UWEKEZAJI KATIKA MAENEO YA KALE WARUHUSIWA NA MALIASILI

Wizara ya Maliasili na Utalii imefafanua kuwa kwa mujibu wa
 Sera ya Malikale ya mwaka 2008 (Kifungu cha 4.5 na 46),
 wananchi, taasisi mbalimbali, pamoja na wadau wengine wa 
uhifadhi wanaruhusiwa kumiliki, kulinda, kuhifadhi na 
kuendeleza urithi wa utamaduni nchini kwa manufaa ya
 kizazi cha sasa na kizazi kijacho kwa sababu za mafunzo, 
historia na utalii. Sera pia inaruhusu uwekezaji katika
 maeneo ya malikale ambao unalenga kuhifadhi na
 kutumia rasilimali za malikale kama vivutio vya utalii.

Ufafanuzi huu umetolewa kufuatia habari iliyoandikwa
 na gazeti moja la kila siku kuhusu mwekezaji kumilikishwa
 isivyo halali eneo lenye magofu ya kihistoria la kisiwa cha
 Chole kilichopo wilayani Mafia ambayo sasa yanatumika
 kama sehemu ya hoteli ya kitalii.

Wizara kupitia Idara ya Mambo ya Kale inatambua kuwa
 magofu ya kihistoria katika kisiwa cha Chole ni
 Kumbukumbu za Urithi wa Utamaduni yenye umuhimu
 kitaifa na kimataifa na Magofu haya yanalindwa na Sheria
 ya Mambo ya Kale Na. 10 ya mwaka 1964 na
 marekebisho yake Na 22 ya mwaka 1979. Idara inawajibika
 kusimamia uhifadhi na uendelelezaji wake kulingana
 na kanuni na miongozo ya uhifadhi na uendelelezaji.

Wizara inasisitiza kuwa siyo maeneo yote ya urithi wa
 utamaduni yanasimamiwa na Idara ya Mambo ya
 Kale moja kwa moja. Maeneo ya urithi wa utamaduni
 yenye sifa za kitaifa ni mengi lakini 12 tu ndiyo yanayomilikiwa
 na Serikali Kuu na kuendelezwa na Idara ya Mambo ya Kale.
 Maeneo yaliyo mengi yanamilikiwa na watu binafsi,
 taasisi za umma na binafsi na vijiji au wilaya. 
Kwa mfano, Magofu ya Chole, Mafia hayapo chini ya
 umiliki wa Idara ya Mambo ya Kale moja kwa
 moja bali yapo chini ya umiliki wa wilaya 
na serikali ya kijiji cha Chole.

MHH KUNANI TENA SEPETU NA JB



TREY SONG AMPIGA KIBAO NDUGU YAKE KIM KARDASHIAN

The r&b singer trey songz ambaye kwa sasa anafanya poa na  heart Attack

 kutoka kwenye album yake ya nne

 anayotarajia kuereleas mwezi june tarehe 26 inayokwenda kwa jina la

 Chapter V, amemzaba kibao moja ya wanafamilia wa Kim Kardashian

 anayefahamika kwa jina la Rob Kardashian, chazo kinasema kuwa

 Rob na ndugu zake walikuwa pande za  London kwenye nightclub

 inayofahamika kwa jina la  MOVIDA nightclub  wakiwa wamekaa

 VIP section  wakiendelea na uchukuwaji wa Video ya kipindi chao cha

 reality show, mara ghafla R&B singer Trey aliiingia eneo lile akiwa na

 watu wapatao kumi na alipofika eneo lile mara baada ya kuona shughuli ya

 uchukuwaji vidio likiendele alijaribu kuwasiliana na uongozi na kupewa

 jibu kuwa hawakuwa na taarifa hiyo ndipo Trey aliwaamuru familia hiyo

 ya Kardashian Kutoka nje mara moja coz heneo hilo lilitengwa kwa ajili yao

 ila baadae Rob alijua Trey anjok ndipo alipojaribu kumfuata kwa lengo

 la kumpliz ili waendele na shughuli yao likini alikutana na ali tofauti

 kwani inasemekana trey alimzaba Kibao nandipo Rob aliwaamuru Ndugu 

zake na watu aliokuja nao kutoka nje, Bado mpaka sasa Familia ya

 Kardashian haija zungumza chochote kuhusiana na swala hili so

 tuendelee kusikilizia…..


DJKHALED KUTOKA NA KISS THE RING

Mara baada ya kufanya poa na album ya "We the Best Forever." (2011)
 Ambayo ilikuwa na Hit singo kama “welcome to My Hood” na  
 “ I’m On One” ambayo amemshirikiha Rick Ross na Drake
 hatimaye sasa Dj maarufu Duniani mtumzima Dj Khaleed
 ameamua kudondoka tena mwaka huu na Album nyingine aliyoipachika
 jina la “Kiss the Ring” ambayo amepanga kuidrop sikono mwezi
 August 21st  na tayari mpaka sasa Dj huyo kutoka pande za  Miami, Florida
 ameshaanza kufanya  promotional  title  ya video ya 
Album yake hiyo Mpya ya “Kiss the Ring  ambayo
 ameifanya kwa ushirikiano wa  YMCMB pamoja na 
We The Best Music Group. Album hii itakuwa ni ya tano
 kwa mtumzima Dj Khaleed tangu alipoanza kutoa
 album yake ya kwanza mwaka 2006 iliyokwenda kwa jina la 
“Listen.. the album