Ghasia zimezuka mjini Mombasa baada ya mhubiri wa kiisilamu
ambaye
pia alikuwa mshukiwa wa kufadhili kundi la wanamgambo la
Al shabaab
nchini Somalia, Aboud Rogo, kuuawa kwa kupigwa
risasi mjini Mombasa pwani mwa
Kenya.
Mtu mmoja inaarifiwa ameuawa na wengine kujeruhiwa
katika mtaa wa Mejengo
kufuatia makabiliano kati ya polisi
na mamia ya watu walioghadhabishwa na
kitendo cha kuuawa
kwa bwana Rogo ambaye alikuwa mhubiri wa kiisilamu mjini
Mombasa
Hali ingali tete wenye maduka wakilazimika kuyafunga
maduka yao na watu
kukimbilia usalama wao katika mtaa
wa Majengo katika maeneo ya kati ya mjini
Mombasa.
Inaarifiwa Aboud Rogo,alipigwa risasi asubihi ya leo na
kuaawa wakati
alipokuwa akimpeleka mke wake hospitalini
katika mtaa wa Bamburi mjini
Mombasa.Watu wamechoma
magari na hata kuvamia maduka huku hali ya wasiwasi
ikitanda polisi nai wakifanya kila hali kuweza kutuliza mambo.
Duru zinaarifu kuwa huenda Rogo aliuawa na polisi
ingawa ripotio hizi bado
hazijathibitishwa.
Anasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake
ambalo lilikuwa
limewabeba watu wengine sita,
alizikwa baadaye saa za mchana.
Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya umiliki haramu
wa silaha ambapo
polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya
kushambulia kanisa moja la kikatoliki
mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya
Marekani na ile ya Umoja wa
mataifa ya watu wanaosaidia
katika harakati za kundi la wanamgambo wa kiisilamu
nchini
Somalia la al-Shabab
Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo alisaidia kundi la
al-Shabab
kusajili makurutu wapya. Pia alikuwa anakabiliwa na
madai ya njama ya
mashambulizi dhidi ya kanisa moja mjini Mombasa.
Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo alipigwa risasi wakati
akiendesha gari lake
katika mtaa a Bamburi mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed aliwekwa nwenye oriodha ya
Marekani ya watu waliowekewa
vikwazo mwezi Jilai,kwa
kujihihusisha vitendo vyinavyohujumu amani na usalama
nchini Somalia.
Wapiganaji wa al Shabaab
Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilimwekea vikwazo
vya usafiri na pia
kupiga tanji mali zake mwezi Julai, wakisema
kuwa alitoa ufadhili wa kifedha,
usafiri na kusaidia kundi
hilo kwa vifaa vya kisasa.
Ilimtuhumu kwa kuwa kiongozi maalum wa vuguvugu la
al- Hijra nchini Kenya
ambao pia wanajulikana kama
Muslim Youth Center, ambalo linatazamiwa na wengi
kama lililo na uhusiano wa karibu na al-Shabab.
Umoja wa mataifa ulisema kuwa bwana Rogo alitumia kundi
hilo kama njia moja
ya kuwatia watu kasumba ya siasa kali hasa
wanaoongea lugha ya kiswahili kwa
lengo la kufanya
mashambulizi ya kigaidi.
picha na stori kwa hisani ya bbc